ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea kwa ukali wakati
akionyeshwa ramani na Mpima wa Manispaa Selice Nzyungu ya eneo
alilouziwa muwekezaji Ephatta Ministry na lile walilopewa wananchi wa
kata ya Mollo katika Manispaa ya Sumbawanga. Mkuu huyo wa Mkoa
amelazimika kutembelea eneo hilo baada ya kupewa taarifa za awali na
Kamati aliyoiunda katika kufuatilia mgogoro unaoendelea kati ya
muwekezaji na wananchi wanaolizunguka shamba hilo. Lengo kuu la ziara
yake hiyo ya tarehe 02, Septemba 2012 ilikuwa ni kutembelea mashamba
yakiwemo ya muwekezaji na wananchi pamoja na kuzungumza na wananchi na
muwekezaji kwa kuchukua kero zao kwa ajili ya kuutafutia ufumbuzi
mgogoro huo.
Mkuu
huyo wa Mkoa wa Rukwa akizungumza kwenye Mkutano na wananchi wa kata ya
Molo ambapo pia wawakilishi wa muwekezaji walialikwa kuskiliza na kutoa
kero zao mbele ya wananchi wa kata hiyo. Hata hivyo baada ya Mkuu huyo
wa Mkoa kusikiliza kero hizo aliwaahidi wananchi pamoja na muwekezaji
kuendelea kuushughulikia Mgogoro huo kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata,
Wilaya, Mkoa, Wizara na Taifani kwa ujumla kwa ustawi wa wote na
maendeleo ya Mkoa na Nchi kwa ujumla. Alisema kuwa lengo lake sio
kuegemea upande mmoja bali ni kutafuta haki kwa kila pande. Aliwataka
wananchi na muwekezaji kufungua upya milango ya mahusiano mazuri baina
yao ili kumuunga mkono katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo ambao
umekuwa ukiibua sura mpya kwa vipindi tofauti.
Wananchi
wakitoa kero zao mbalimbali zikiwepo unyanyaswaji kwa kuchapwa viboko
na kukatwa maskio kwa pindi wakutwapo na muwekezaji huyo wakipita
shambani kwake au wakikata nyasi kwa ajili ya kulishia mifugo yao. Kero
nyingine waliyoitoa ni kukosa maeneo ya kulima na kupata kipato kutokana
na eneo kubwa kupewa muwekezaji ambalo eneo alilopewa ni hekta alfu
kumi (10,000) kwa ajili ya ufugaji kwa mujibu wa Mkataba. Uharibifu wa
barabara pamoja Muwekezaji huyo kwenda kinyume na Mkataba wake wa kufuga
na badala kulima zaidi ni kero pia ambayo waliitoa wananchi hao wa kata
ya Molo.
Ndugu
Josephat Mutarabuga ambaye ni muwakilishi na mfanyakazi wa Ephata
Ministry Heritage Pharm linalomiliwa na Ephata Minisrty akitoa kero za
muwekezaji huyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambazo ni uharibifu wa
wananchi kwenye shamba lao. Alisema kuwa wananchi wa Vijiji vya
mawenzusi wamekuwa wakichoma moto mashamba yao hali inayopelekea
uharibifu mkubwa wa mazao yao. Alisema pia kuwa wananchi wa vijiji hivyo
hukata pia mazao ya mahindi ambayo bado ni mabichi kula Migagi (Kula
mashina ya Mahindi kama miwa)
Sehemu ya wananchi, viongozi wa serikali na wawakilishi wa muwekezaji wakiwa kwenye Mkutano huo uliofanyika tarehe 02, Septemba 2012.
Sehemu ya wananchi, viongozi wa serikali na wawakilishi wa muwekezaji wakiwa kwenye Mkutano huo uliofanyika tarehe 02, Septemba 2012.