BIA RUHUSA KOMBE LA DUNIA BRAZILI
Rais wa Brazil Dilma Rousseff amesaini kuwa sheria muswada utakaoruhusu uuzwaji wa bia wakati wa mechi za Kombe la Dunia mwaka 2014. Rais wa Brazil akiwa na viongozi wa Fifa pamoja na Pele Shirikisho la Kandanda Duniani, Fifa, lilikuwa linataka mabadiliko katika sheria ya Brazil inayopiga marufuku pombe kuuzwa kwenye mechi za mpira wa miguu. Muswada huo mpya, umeweka sheria kadha kwa ajili ya Kombe la Dunia, haujaelezea kuweka pingamizi lolote la kuuzwa pombe. Waandishi wa habari wanasema magavana wa majimbo bado wanaweza kupiga marufuku uuzwaji wa bia wakati wa mashindano hayo. Uuzaji bia umekuwa mwiko katika mechi za kandanda nchini Brazil tangu mwaka 2003. Upigwaji huo marufuku uliwekwa ikiwa ni sehemu ya hatua ya kupambana na vurugu miongoni mwa mashabiki wa timu zenye uhasama pamoja na kukabiliana na wahuni...