KESI YA LULU YASOGEZWA HADI JUNI 25


WAKILI mmoja wapo anayemtetea  Elizabeth Michael  Fulgence Massawe akimsalimia ''maarufu kama  Lulu'' kabla Jaji Dk. Fauz Twaibu hajaingia Mahakamani juzi asubuhi katika Mahakama Kuu ambako kesi hiyo ilipigwa tena kalenda hadi Juni 25 mwaka huu. Pia Jaji Fauz amezitaka pande zote mbili yaani Wakili wa Serikali pamoja na Jopo la Mawakili wanaomtetea  kupeleka vuthibitisho kuhusiana na umri wa Lulu Mahakamani hapo.

MAHAKAMA Kuu kanda ya Dar es Salaam imewataka mawakili wa utetezi na jamhuri kuwasilisha uthibitisho kuhusu umri wa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ kabla ya kutoa uamuzi wake Juni 25, 2012.

Agizo la Mahakama hiyo lilitolewa juzi na Jaji Dk. Fauz Twaib anayesikiliza madai ya utata wa umri wa msanii huyo nyota wa maigizo nchini.

Kabla ya kuahirisha kesi hiyo Jaji Dk. Twaib alizitaka pande mbili zinazobishana kupeleka vithibitisho vya hati ya kiapo cha cheti cha kuzaliwa ili kujiridhisha umri sahihi wa Lulu.

Kwa upande wake wakili wa mshitakiwa Flugency Massawe alidai mahakamani hapo kwamba hadi Juni 13 atakamilisha vithibitisho hivyo wakati wakili wa serikali Elizabeth Kaganda alidai kazi hiyo ataikamilisha Juni 22 mwaka huu.

Lulu anayetuhumiwa kwa mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba ''the great'' Aprili 7 mwaka huu anadaiwa kuwa chini ya miaka 18 huku jamhuri wakidai kwamba mshtakiwa huyo ana zaidi ya umri huo.

 Pamoja na Massawe mawakili wengine wanaomtetea msanii huyo ni Jacqueline Dimelo, Kennedy Fungamtama na Maico Kibatala huku Shadrack Kimaro na Kaganda wakiongoza kesi hiyo upande wa jamhuri.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA