MWENGE WAWASILI ZANZIBAR
Mwenge wa Uhuru leo Umeingia Kisiwani Zanzibar ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Kapteni Honest Mwanossa ameweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo katika mkoa wa mjini Magharibi. Akiweka jiwe la Msingi la kituo kidogo cha Polisi cha Kombeni Mjini Zanzibar, kiongozi huyo amewataka viongozi wa Kitaifa kuepuka ufujaji wa fedha za wananchi na kujiingiza kwenye ufisadi na kuwataka wafanye mambo kwa maslahi ya Taifa. Awali katika risala yao kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge, wananchi wa Makombeni wameliomba Jeshi la Polisi kuangalia uwezekano wa kuharakisha ujenzi wa kituo hicho ili kupunguza kero ya uhalifu katika eneo hilo. Moja ya ujumbe wa Mwenge wa mwaka huu umehimiza umuhimu wa kila mmoja wetu kuhesabiwa katika Sensa ya kitaifa ili kuiwezesha Serikali kupanga vema maendeleo kwa wananchi wake. Mwenge huo umewasili kisiwani Zanzibar ukiotokea mkoa wa Lindi ambako ulikuwa ukikimbizwa katika wilaya mbalimbali za mkoa h...