TSN HAIJAMTELEKEZA ATHUMANI HAMISI
Tarehe 5 Juni,2012, mfanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), ambaye amelemaa baada ya kupata ajali ya gari, Bwana Athumani Hamisi, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Maelezo, Dar es Salaam, na kutoa taarifa iliyojenga taswira kuwa ametelekezwa na TSN pamoja na Serikali. TSN inapenda kufafanua kuwa Serikali na kampuni hii, ambayo ilimwajiri Athumani tarehe 1/09/2006 kama Mpiga picha Mwandamizi, wamemhudumia mfanyakazi huyo kikamilifu tangu alipopata ajali tarehe 12 Septemba, 2008 hadi sasa, na huduma hiyo inaendelea. Baada ya kutokea ajali hiyo, TSN kama mwajiri ilisimamia matibabu yake ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI) mpaka Serikali, kwa kupitia Wizara ya Afya ilipomhamishia Netcare Rehabilitation Hospital nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Serikali ililipia gharama za matibabu yake yote akiwa Afrika Kusini kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi saba, ambayo yanazidi shilingi milio...