MAMLAKA ya maji safi na maji taka Jijini Arusha(AUWSA ),imebaini
kuhujumiwa wa watu mbalimbali wakishirikiana na wafanyakazi wake,
wasio waaminifu kwa kuunganisha maji kinyume cha utaratibu na
kusababisha upotevu mkubwa wa mapato.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa AUWSA, Eng.Ruth Koya alisema kuwa,
tayari wamefanikiwa kuwanasa wezi wa maji zaidi ya 100
waliojiunganishia kinyume na utaratibu, wakiwemo vigogo wa
halimashauri ya Arusha,ambao wamekuwa wakitumia huduma hiyo kwa
kipindi kirefu,bila kulipa chochote na kuisababishia hasara kubwa
mamlaka hiyo.
Vigogo wa halmashauri waliokamatwa ni pamoja na Afisa mali asili,
mazingira na ardhi, Maico Myairwa ambaye yeye aling’oa kabisa mita ya
idara ya maji, ambayo imekutwa chumbani mwake, ameificha huku akijua
ni kosa kisheria.
Mwingine ni fundi mkuu wa maji wa halmashauri ya Arusha,Loishono
Mollel ambaye amejiunganishia maji baada ya kutoboa bomba kubwa la
idara ya maji na kupitisha mpira mrefu kwa chini, hadi nyumbani kwake
ambapo pia alikuwa akiyatumia maji hayo kustawisha bustani yake