ZITTO AIBUKA NA JIPYA
MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA), jana aligeuka mbogo na kuwafukuza watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Nchini (Tawiri) baada ya kubaini kupotea kwa silaha ambazo hadi sasa hazijulikani ziliko. Zitto akiungwa mkono na wajumbe wa kamati hiyo, alisema kamati hiyo imepata hofu kubwa juu ya kutoweka kwa bunduki hizo, na zaidi baada ya kubainika kuwa moja ya silaha zinazoaminika kumilikiwa na taasisi hiyo kuhusishwa na tukio la mauaji mjini Mugumu, mkoani Mara. Mbali na kuwafukuza watendaji wa taasisi hiyo, aliwaagiza kuwasilisha haraka ndani ya wiki mbili, ripoti kamili itakayoeleza kinagaubaga namna silaha hizo aina ya bunduki zilivyotoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu mwaka 1980. Zitto alisema kuwa suala la upotevu wa silaha hizo, na nyingine kuhusika katika matukio ya kihalifu ni nyeti, na hivyo kamati hiyo ya Bunge inahitaji maelez...