AHADI KUTOKA CCM
CHAMA cha Mapinduzi, kimesema ahadi ilizozitowa kwa wananchi katika
kuinadi Ilani ya chama hicho inazitekeleza kwa hatua ili kuwaletea
wananchi maendeleo katika maeneo yao.
Aidha chama hicho, kimesema kinakusudia hadi kufikia mwaka 2015 iwe
tayari yake ya Uchaguzi wa mwaka 2010-2015 za kuwaletea Maendeleo, zipo
pale pale na itaendelea kufanya hivyo na kuhakikisha kuwa kero mbali
mbali zinapatiwa ufumbuzi mapema iwezekanavyo kabla ya 2015 hatuwa kwa
hatuwa.
Akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Mkanyageni Pemba, Mjumbe wa Kamati
kuu ya CCM, na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia , Profesa,
Makame Mnyaa Mbarawa, wakati wa kukabidhi mashine ya kusukumia maji kwa
wananchi wa Jimbo hilo, alisema kuwa CCM, ina kila sababu ya kufanya
hivyo kwa kuwa ndicho chama kinachoiongoza nchi.
Alisema huduma nyingi za kijamii ikiwemo, barabara, maji safi na salama,
afya, miradi ya elimu imeweza kutekelezwa kwa kupitia ilani ya chama
hicho cha kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM Taifa, alisema CCM, haijakata tamaa ya
kutotekeleza ahadi zilizobaki ikiwa ni kuwaenzi wapiga kura wa Jimbo
hilo na hata waliokuwa hawakupiga kura.
“ Tuna kila sababu ya kuwaleteeni Maendeleo katika Jimbo hili kwa kadri
inavyowezekana hatuwa bada hatuwa kwa vile sisi ni wananchi wa Jimbo
hili na maendeleo ya hapa yataletwa na sisi wenyewe hatokei mwengine
akatuletea “ alieleza Profesa Mnyaa.
Aliendelea kusema kuwa CCM, ipo kwa ajili ya watu na ipo kwa ajili ya
maendeleo , hivyo aliwataka Viongozi wengine kushirikiana na wale
wenyenia ya kuletea maendeleo kwa Wananchi kwa vile Ustawi wa Wananchi
ni kuwepo maendeleo katika sehemu zao wanazoishi.
Mnyaa, alieleza kuwa kila Mwananchi wa Jimbo hilo watahakikisha kuwa
anafikiwa na maendeleo mbali mbali katika mahala alipo yakiwemo Maji,
Afya , Elimu , Barabara n.k kwa vile ni wajibu wao kama viongozi.
"Sisi hatuna tatizo wala hatua nongwa kwa vile Wananchi wa Jimbo hili
nawakuwa na kura nyingi , lakini tutahakikisha kuwa Mkanyageni inakuwa
na maendeleo ya kutosha,”alisema.
Hata hivyo, aliwataka Vijana wa Jimbo hilo kuwa wabunifu wa maendeleo
ili kuisaidia Serikali katika harakati zake za kuwaletea wananchi
maendeleo kwa kujitokeza katika kazi mbali mbali za ujenzi wa taifa.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Meja mstaafu, Juma Kassim Tindwa,
alimpongeza mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM, kwa juhudi zake za kuleta
maendeleo kwa wananchi wa Jimbo hilo, na kuwataka wananchi hao kuyalinda
na kuyathamini maendeleo hayo.
“ Ni vyema wananchi wa Jimbo la Mkanyageni, mukaona kuwa maendeleo
yaliopo katika jimbo lenu ni yenu wenyewe , kwa maana hiyo muyalinde na
musikubali kuja mtu kuyaharibu” alisema Tindwa.
Kwa upande wake, Afisa mdhamini wa nWizara ya Ardhi , Makaazi , Maji na
Nishati Pemba, Hemed Salim, aliwahakikishia wananchi wa Jimbo hilo
kufaidika na huduma hiyo ndani ya wiki moja kuanzia sasa kwa kuwa vifaa
vyote vimekamilika na vimeshakabidhiwa .
Mashine hiyo ya Maji aliyoikabidhi Profesa Mnyaa kwa wananchi ina
thamani ya shilingi milioni 19 na ina uwezo wa kufanya kazi kwa muda wa
miaka 20.