SPIKA WA BUNGE AWASILI CANADA MJINI QUEBEC
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika uwanja wa ndege mjini Quebec, Canada tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 127 wa chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaotarajia kufunguliwa rasmi kesho tarehe 21 Oktoba, 2012 na kumalizika 26 Oktoba . Makinda ameongoja ujumbe wa wabunge wanne kutoka Tanzania, ambapo zaidi ya maspika wa nchi 150 duniani wakiongoza ujumbe wa wabunge kutoka Nchi zao watashiriki mkutano huo. Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiteta jambo kuhusu maandalizi ya awali ya mkutano na afisa kutoka Bunge la Canada mara alipopokelewa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege mjini Canada kuhudhuria mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani. Kulia ni Mhe. David Kafulila na Mhe. Hamad Rashid waliongozana na Mhe. Spika katika Mkutano huo nchini Canada Mhe. Spika Anne makinda na ujumbe wake wakionyesha nyaraka muhimu za kusafiria kwa ofisa wa uwanja wa ndege mara baada ya kuw...