FRANCIS CHEKA VS BENJAMIN SIMON NOVEMBER 18, 2012
Mpambano unaosubiriwa kwa hamu
kubwa na wadau wa ngumi nchini Tanzania na Ujerumani kati ya Francis
Cheka na Benjamin Simon wa Ujerumani sasa utafanyika tarehe 18 November
katika ukumbi wa Universal jijini Berlin nchini Ujerumani.
Awali mpambano huo ulikuwa
ufanyike tarehe 17 November jijini Berlin, Ujerumani na tayari bondia
Francis Cheka ameshasaini mkataba wa kukutana na mbabe huyo wa Ujerumani
anayejulikana kwa jina la “Iron Ben” kwa ajili ya ukali wa makonde
yanayowasulubu wapinzania wake.
Mtanzania bondia Francs Cheka
Bondia Benjamin Simon ana
rekodi ya mapambano 24 ambapo amepoteza pambano moja wakati bondia
Francis Cheka ana rekodi ya mapambano 33 amepoteza mapambano 6.
Bondia Benjamin Simon wa Ujerumani
Akimwandikia “Eva Rolle” wa
kampuni ya “Primetime Event Management” ya Ujerumani ambaye ndiye
promoter wa mpambano huo, mwenyekiti wa ubingwa wa IBF/USBA Lindsey
Tucker alimfahamisha kuwa Rais wa IBF/USBA Daryl Peoples au yeye
mwenyewe Lindsey Tucker watawasiliana na mama huyo kuhusu maofisa
watakaosimamia mpambano huo.
Hii itakuwa
mara ya kwanza kwa wababe hao kukutana kugombea mkanda wa IBF wa mabara
(IBF I/C) na mpambano wao unategemnea kutoa ushindani mkubwa.
Mshindi katika mpambano huo ataingia moja kwa moja katika orodha ya mabondia 15 bora kwenye uzito wa Super Middle duniani.