Wazalishaji Wa Chumvi Bagamoyo Walalamikia Kupanda Kwa Ushuru
by David Mathias WAZALISHAJI wa Chumvi katika Wilaya ya Bagamoyo wamelalamikia ongezeko la ushuru wa chumvi unaodaiwa kupanda kwa asilimia 50 zaidi ya kiwango kilichokuwa kikitozwa hali inayowasababishia kuongezeka kwa gharama za uzalishaji kuliko bei halisi ya masoko. Malalamiko hayo yametolewa mwishoni mwa wiki na Katibu wa Chama cha Wazalishaji Chumvi Tanzania (TASPA), Julius Mosha wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa kuhusiana na malalamiko yanayotolewa mara kwa mara na wadau wa sekta ya chumvi. Mosha alisema kuwa mwaka 2008 Halmashauri hiyo ilipitisha sheria ndogo ya ongezeko la ushuru wa chumvi toka kutoka Sh.50 kwa mfuko wa kilo 50 sawa na Sh,1000 kwa tani, ikafikia Sh.200 kwa mfuko wa kilo 50 sawa na Sh.4000 kwa tani, hata hivyo ongezeko hilo lililalamikiwa sana na kudai kuwa inashangaza licha ya kuwa na malalamiko hayo kuna taarifa nyingine ya ongezeko la asilimia 50 zaidi. Alisema...