SERIKALI IMESEMA HAIJADHULUMU MALIPO YA WAHANGA
SERIKALI imesema kuwa hakuna malipo ya kiasi kidogo cha fedha kilicholipwa kwa waathirika wa mlipuko wa mabomu ya Kambi ya jeshi ya Mbagala yaliyotokea mwaka 2009 kama ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila wiki la hapa nchini hivi karibuni. Akizungumza na Idara ya Habari( MAELEZO) jana ofisi kwake , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema hakuna fidia ya Shs. 1400 na Shs. 2500 iliyotolewa kuwa ni ya uharibifu wa jumla ya fidia za malipo kwa wahanga hao, bali malipo hayo ni tofauti ya kiasi cha fedha kilichokuwa kinadaiwa na wahanga hao ambacho kilichobakia. ‘’ Unajua malipo ya wahanga hao yalifanyika katika awamu mbili. Hivyo kiasi cha fedha cha malipo hayo yaliyotolewa katika hundi hizo , ambayo iliripotiwa katika gazeti hilo ni malipo ya awamu ya tatu. Malipo hayo ni tofauti ya fedha kilichokuwa kinadaiwa na si kweli kuwa wahanga hao walilipwa fed...