SERIKALI IMESEMA HAIJADHULUMU MALIPO YA WAHANGA
SERIKALI imesema kuwa hakuna malipo ya kiasi
kidogo cha fedha kilicholipwa kwa waathirika wa mlipuko wa mabomu ya Kambi ya jeshi
ya Mbagala yaliyotokea mwaka 2009 kama ilivyoripotiwa na
gazeti moja la kila wiki la hapa nchini hivi karibuni.
Akizungumza na Idara ya Habari( MAELEZO) jana ofisi kwake ,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema hakuna fidia ya Shs.
1400 na Shs. 2500 iliyotolewa kuwa ni ya
uharibifu wa jumla ya fidia za malipo kwa wahanga hao, bali malipo hayo ni
tofauti ya kiasi cha fedha kilichokuwa kinadaiwa
na wahanga hao ambacho kilichobakia.
‘’ Unajua malipo ya wahanga hao yalifanyika katika awamu mbili. Hivyo
kiasi cha fedha cha malipo hayo yaliyotolewa katika hundi hizo
, ambayo iliripotiwa katika gazeti hilo ni malipo ya awamu ya tatu.
Malipo hayo ni tofauti ya fedha kilichokuwa
kinadaiwa na si kweli kuwa wahanga hao walilipwa fedha hizo kama jumla
ya fidia za malipo yao,’’ alifafanua Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu huyo wa Mkoa, aliongeza kuwa habari hiyo iliyoandikwa sio sahihi na haikufuata maadili ya uandishi
wa habari kwani hakuweka wazi usahihi wa taarifa hiyo.Serikali haijamdhulumu mtu yeyote, bali inalipa kutokana malipo stahili.
‘’Ninaomba waandishi wa habari waandike habari
walizozifanyika utafiti wa kina wa pande zote ilikuepusha utoaji wa taarifa
zisizosahihi,’’ alisisitiza.
Aidha Mkuu huyo alisema malipo ya waathirika hao yanatolewa
kwa awamu tofauti na kwa idadi ya watu maalum, kwa sababu ya kuepusha utoaji wa
malipo yasiyostahili. Hivyo aliwataka waathirika hao kuvuta subira kwa
kuwa malipo hayo bado yanaendelea.