SERIKALI ITALINDA AMANI KWA NGUVU ZAKE ZOTE
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein ,alipokuwa akizungumza na Wahariri na Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Bara na Visiwani,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Na Juma Mohammed, MAELEZO Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema kwamba Serikali italinda amani kwa nguvu zote na kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaochochea na kufanya vurugu. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar jana,Dk. Shein alisema “Tutailinda amani kwa nguvu zote, atakayethubutu kuchezea tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria” Rais Shein alisema amesikitishwa sana na vitendo vilivyotokea wiki iliyopita na kuelezea vurugu hizo zimeharibu sifa njema ya Zanzibar ambayo kwa miaka mingi ianjulikana kwa uvumilivu wa kidini kiasi cha hata Serikali ya kikoloni mwaka 1953 kuamua kufanya shindano...