OKWI KUUZWA SIMBA KWA SH. BILIONI 2

UONGOZI  wa Klabu ya Simba umewataka baadhi ya watu kuacha tabia ya kutaka
kutangaza kuwa wanamchukua mchezaji Emmanuel Okwi wakati wakijua ni mchezaji halali wa klabu hiyo.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa kuna baadhi ya watu wameanza kutumia jina la Okwi kama njia ya kupata uongozi au kuonekana bora katika klabu zao huku zikiwa hazijawahi hata siku moja kufanya maongezi na klabu ya Simba.
Alisema kama kuna klabu inataka kumsajili mchezaji huyo ifuate utaratibu wa kuongea na viongozi wake kwa kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya Simba.

Aliongeza kuwa kama kuna mtu au klabu inataka imsajili Okwi inatakiwa kutumia zaidi ya bilioni 2 ili iweze kumchukua.
Alisema mchezaji huyo anatakiwa katika mabala ya ulaya kama Tanzania kuna mtu anauwezo wa kutoa fedha hiyo klabu ya Simba ipo tayari kumuuza kwa pesa hiyo.
"Tupo tayari kumuuza kama kuna klabu hapa nchini ina bilioni 2, sisi tunamuachia kwa kuwa bado mchezaji wetu na anaendelea kuitumikia klabu yetu ya Simba kwa zaidi ya miaka miwili"alisema Kamwaga.

Klabu ya Yanga kupitia wadau wake juzi ilitangaza kumchukua mchezaji huyo raia wa Uganda kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA