MKATABA
Serikali ya Tanzania na serikali ya Jamhuri ya watu wa China kesho (18/06/2012) zinatarajia kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa Bomba la kusafirisha Ges asilia kutoka Mnazi Bay Mtwara hadi Ubungo jijini Dar es Salaam. Mkataba huo wenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 2 (mbili) utasainiwa mjini Beijing, China kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini kwa upande wa Tanzania (TPDC) na Benki ya Exim kwa upande wa China. Balozi wa Tanzania nchini China Mhe Phillipo Marmo amesema hayo leo mjini Wuhan, China wakati akizungumza na Umoja wa Wanafunzi wa Tanzania (Wuhan Tanzania Students Association-UTASA) wanaoishi mjini hapo. "Kesho Tanzania inatarajia kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Mnazi Bay Mtwara hadi Ubungo jijini Dar es Salaam utakaokamilika ndani ya mezi 12 baada ya kutiwa saini," amesema. Kwa mujibu wa Balozi Marmo, "serikali ya Tanzania imeiwekea dhamana PTDC ili kupata mkopo kutoka benki ...