KALALA JUNIOUR ARUDI
BAADA YA KUONDOKA MAPACHA WATATU, HAPA NDIPO ALIPOHAMIA KALALA JUNIOUR! Millard Ayo na Kalala Juniour Mkali wa muziki wa dance ambae alikua kwenye familia ya band ya MAPACHA WATATU Kalala Juniour leo ametangazwa rasmi kujiunga na AFRICAN STARS TWANGA PEPETA. Kwa zaidi ya mwezi mmoja kulikua na stori kibao mtaani kwamba Kalala baada ya kugawana shea na Mapacha atajiunga na Mashujaa Band lakini haijawa hivyo. Baada ya kutambulishwa leo amesema hajalazimishwa kujiunga Twanga ila ni mapenzi yake tu kurudi kwenye band hiyo aliyoifanyia kazi kabla ya Mapacha. Amesema koti lilimbana Mapacha ndio maana akaamua kulivua, sasa hivi toka amehamia Twanga tayari amesharekodi nyimbo mbili ikiwemo moja inaitwa ‘nyumbani ni nyumbani’