TANZANIA KUTOUZA GESI ASILIA NJE YA NCHI HADI IJITOSHELEZE MAHITAJI YA NDANI
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akongea wakati wa mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini. Nyuma yake mwenye laptop ni Meneja wa Sekta Kupunguza Umaskini na Kusimamia Maendeleo ukanda wa Afrika wa Benki ya Dunia Dkt Albert Zeufack, akiwa ameongozana na mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na Timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo na inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani ****** YALIYOSEMWA NA KATIBU MKUU KIONGOZI LEO WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI Katika miaka ya karibuni kumekuwepo kwa ugunduzi mkubwa wa gesi asili nchini Tanzania katika maeneo ya mwambao na maeneo ya kina kirefu cha bahari ambapo mpaka sasa jumla ya futi za ujazo trilioni 33 zimegunduliwa. Kazi ya utafutaj...