SHEIKH FARID AREJEA NYUMBANI KWAKE SALAMA
Kiongozi
wa Jumuiya ya Uamsho visiwani Zanzibar, Sheikh Farid, (Wapili kushoto),
akipiga picha ya ukumbusho na familia yake mara baada ya kjuwasili
nyumbani kutoka kusikojulikana, Ijumaa Oktoba 19, 2012
Sheikh Farid, akipokewa na ndugu na jamaa nyumbani kwake
Sheikh Farid, na baadhi ya wafuasi wake, wakiomba dua nyumbani kwake mara baada ya kupatikana, Ijumaa Oktoba 19, 2012 |
Kuna habari kuwa
kiongozi wa Jumuiyab ya Uamsho, kisiwani Unguja, Zanzibar, Sheikh Farid
amepatikana nay u salama salimin.
Picha za mitandao
zinaonhyesha sheikg huyo mwenye msimamo makali alionekana akilakiwa na watu b
waliotajwa kuwa ni ndugu na jamaa, ambapo picha nyingine zinaonyesdha akiwa na
familia yake na moja ikionyesha akiomba dua nyumbani kwake.
Kwa mjujibu wa taarifa
za mkitandao, Sheikh huyo aliyetoweka tangu Oktoba 16, 2012 na kuonekana tena
Oktoba 19, 2012 majira ya jioni, alisema, “alichukuliwa na watu
waliojitambulisha kwake, kuwa ni askari polisi na baadhi yao wakiwa na silaha.”.
Alisema
|Nilifungwa kitambaa cheusi
usoni na kupelekwa nisikokujua” alifafanua sheikh huyo.
Amedai askari hao
wenye lafudhi za Tanzania Bara na wengine Visiwani, walitaka kujua kuhusu
harakati zake zikiwemo safari zake za nje zikiwemo za Uarabuni na mahusiano
yake na baadhi ya viongozi wa serikali.
Pia askari hao
walichukua simu yake na kumuhoji mengi kuhusu namba na message zilizopo kwenye
simu yake.
Alisema watu hao waliomchukua kwa gari walikuwa wanne, akiwepo dereva na mwingine aliyekaa mbele ambaye alijitambulisha kwake, na nyuma ya gari walikuwepo watu wawili waliovaa kofia zilizofunika nyuso zao.