WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA MSHINDI WA KWANZA WA SHUGHULI ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2012 KANDA YA IV ILIYOSHINDANISHA MIKOA MITANO
Mkuu
wa Wilaya mpya ya Kalambo Moshi Chang’a ambaye alimuwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwenye shughuli za kuzima Mwenge
wa Uhuru Mkoani Shinyanga akionyesha Kikombe na Cheti alichokabidhiwa na
Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama zawadi ya ushindi kwa Wilaya yake
baada ya kushika nafasi ya kwanza katika shughuli za mbio za mwenge wa
Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya
Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake alipowasili jana
Mkoani Rukwa aikitokea Shinyanga.
Wawakilishi
wa Mkoa wa Rukwa waliokwenda kushiriki kuzima mwenge wa uhuru Mkoani
Shinyanga na kurudi na kikombe cha ushindi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya
ya Kalambo Moshi Chang’a, mratibu wa Mwenge Kimkoa Abubakar Serungwe na
Katibu wa Mkuu wa Mkoan Frank Mateny wakipewa mapokezi na uongozi na
watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akipokea kikombe hicho
cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a muda
mfupi baada ya kumpokea akitokea Mkoani Shinyanga alipokwenda
kumuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwenye kilele cha kuzima mwenge wa
uhuru.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ALhaj Salum Mohammed Chima akifurahia kikombe hicho kwa pamoja na watumishi wenzake.
Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akimpa Mkono wa pongezi Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a kwa ushindi alioupata wa Wilaya yake
mpya kuwa mshindi wa kwanza wa shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka
2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi,
Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa
wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chuma.