Kamati ya Bunge yatembelea Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere


Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam linavyoonekana kwa nje baada ya kukamilika. Jengo hilo linalomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  lipo Makutano ya Barabara za Shaaban Robert na Garden Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (kushoto) akimkaribisha Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.), Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Katibu Mkuu, Bw. Haule akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere walipokitembelea hivi karibuni.
Wajumbe wa Kamati ya NUU na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati akiwakaribisha.
Mhe. Azzan akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya NUU na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje. Kulia ni Balozi Rajab Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje.
Katibu Mkuu, Bw. Haule akitoa maelezo kuhusu Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama waliotembelea kituo hicho 

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA