KASI YA TEKNOLOJIA YAONGEZEKA KWA NCHI ZA AFRICA
KASI YA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA KWA NCHI ZA AFRIKA YAONGEZEKA
KASI ya Maendeleo ya
Teknolojia kwa nchi za Afrika ni kubwa hali inayosababisha baadhi ya
Mashirika ya Viwango nayo kubuni mbinu zitakazoendana na mabadiliko hayo
.
Hayo yalisemwa na Mratibu wa Masuala ya Viwango vya Kimataifa kutoka Shirika la Viwango Tanzania
wakati alipokuwa akizungumzia na waandishi wa habari juu ya Mkutano wa Baraza la Mashirika ya Viwango kwa Nchi za Afrika (ARSO) unatakofanyika Oktoba 22 hadi 24 Jijini Arusha na kushirikisha Nchi 12 kutoka Bara la Afrika.
wakati alipokuwa akizungumzia na waandishi wa habari juu ya Mkutano wa Baraza la Mashirika ya Viwango kwa Nchi za Afrika (ARSO) unatakofanyika Oktoba 22 hadi 24 Jijini Arusha na kushirikisha Nchi 12 kutoka Bara la Afrika.
Bw.Mnunguli amesema hivi sasa kasi
ya ukuaji wa teknolojia ni kubwa katika nchi za Afrika hivyo pia kasi
hiyo ni changamoto kubwa kwa mashirika ya viwango na kuongeza kuwa
mkutano huo utajadili changamoto za viwango pamoja na kubadilishana
uzoefu kwa wataalam wa viwango katika kila nchi za Afrika.
Aidha amesema mkutano huo
utajadili changamoto za viwango pamoja na kuweka mikakati
itakayowezesha wajasiriamali ,wafanyabiashara na kupata maendeleo
kutokana na bidhaa wanazozalisha.
Amesema katika mkutano huo
watapitia katiba pamoja na kuangalia uwezekano wa kubadilishana wataalam
ambao wataweza kufanya kazi kwa muda Nchini Kenya lengo ni kuboresha
matatizo ya viwango.
Mkutano huo utajadili changamoto
mbalimbali zinazokumba mashirika ya viwango ya TBS katika nchi za
Afrika pia tutahakikisha wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara
wanaondokana na vikwazo wanavyokutana navyo.
Naye Afisa Viwango kutoka TBS,
bw.Rocda Andusamile alisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara, Grace Mapunjo anatarajia kufungua mkutano huo na kuongeza
kuwa mkutano huo utashirikisha nchi za Misri, Malawi, Nigeria, Kenya,
Sudani, Rwanda, Ghana, Cameroon, Afrika Kusini, Tunisia,Kongo,
Sudan,Madagascar na Gabon