ZOEZI LA KUKAMATA MAGARI YA SERIKALI YANAYOTUMIA NAMBA BINAFSI KUFANYIKA NCHI NZIMA


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kusisitiza  utaratibu wa usajili wa magari  ya Umma unafuatwa na kutafanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote. Serikali imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba  za kiraia, yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma .  Baada ya hapo Operesheni hiyo iitakamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma,Vilevile kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT,JW, DFP, CW, SM na ,SU.Hadi sasa serikali imesajili vyombo vya moto,123,431 yakiwemo magari,,pikipiki,bajaj na mitambo ya umma. Pamoja nae ni kamansda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi, James Mpinga

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA