SERIKALI ITALINDA AMANI KWA NGUVU ZAKE ZOTE

Na Juma Mohammed, MAELEZO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed
Shein amesema kwamba Serikali italinda amani kwa nguvu zote na kuonya
kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaochochea na kufanya
vurugu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar
jana,Dk. Shein alisema “Tutailinda amani kwa nguvu zote, atakayethubutu
kuchezea tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria”
Rais Shein alisema amesikitishwa sana na vitendo vilivyotokea wiki
iliyopita na kuelezea vurugu hizo zimeharibu sifa njema ya Zanzibar
ambayo kwa miaka mingi ianjulikana kwa uvumilivu wa kidini kiasi cha
hata Serikali ya kikoloni mwaka 1953 kuamua kufanya shindano la uchoraji
wa stamp ya uvumilivu wa kidini.