SIMBA YAJITETEA.
KOcha mkuu wa Simba Milovan Cirkovic na msemaji wa timu hiyo Ezekiel Kamwaga
SIKU moja baada ya kutolewa katika michuano ya Kagame kwa klabu ya Simba, uongozi wa klabu hiyo umewataka mashabiki na
wanachama kutulia kwani kikosi hicho ndio kinasukwa.
Makamu Mwenyuekiti
wa Simba imu hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alisema kikosi cha Simba kinaundwa
na wachezaji wengi wageni hivyo bado timu haijawa katika mfumo mmoja.
Alisema hali hiyo ndiyo ilichangia kufanya vibaya kwa timu
hiyo katika michuano ya Kagame ambapo Simba ilimalizia mbio zake katika hatua
ya robo fainali juzi baada ya kutolewa na Azam Fc kwa mabao 3-1.
“Naomba mashabiki, wanachama na wapenzi wa Simba kuwa
watulivu katika kipindi hichi ambacho naamini kuna mengi yatatokea na hasa kwa
wale wasioitakia mema timu yetu…napenda ieleweke kwamba kocha yupo katika
kupanga kikosi na katika siku zijazo timu itakuwa madhubuti,”alisema Kaburu