ILALA IMEJIPANGA VYEMA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza katika mkutano huo
Wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika mkutano
Hayo yamesemwa na Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mhe. Jerry Silaa katika mkutano wa
kujenga uelewa kwa viongozi kuhusu program ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama
kwenda kwa mtoto.
Akifungua mkutano huo Mhe.
Silaa alisema kuwa Manispaa ya Ilala inashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa malengo ya milenia ya
kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Alieleza kuwa katika Manispaa
ya Ilala kuna vituo mbalimbali vilivyopo katika Hospitali na zahanati kwa ajili
ya kupima virusi vya UKIMWI na kuwapatia wathirika wa UKIMWI dawa za kurefusha
maisha. Alisema kitu muhimu tunachoijikita nacho hivi sasa ni kupunguza
maambukizi ya virusi ya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto.
Alisema kuwa Manispaa ya Ilala ina watalaam wa kutosha wenye uelewa mkubwa wa afya ya Mama na mtoto. ’Ndoto
yetu ni kuwa na kizazi kisicho kuwa na maambukizi ya UKIMWI “ alisema Mhe.
Silaa. Alibainisha kuwa nia ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ni kuwa na
watoto watakaozaliwa bila ya maambukizi ya UKIMWI kufikia mwaka 2015.
Programu hiyo ya kupunguza
maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto inafadhiliwa
na Taasisi ya Management Development to Health (MDH) ambayo imejikita kwenye
mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Akifafanua kazi zianazofanywa
na MDH Dr David Sando ambaye ni Mkurugenzi wa mikakaati ya mawasiliano wa
Taasisi hiyo, alisema kuwa MDH kama mdau
Serikali katika afya imejikita katika kutengeneza miundo mbinu ya afya ,
kujenga Kliniki za kupima maambukizi ya virusi vya UKIMWI pamoja na ukarabati
wa Kliniki hizo.
Alisema kuwa MDH katika
Manispaa ya Ilala wamekuwa wakihakikisha hakuna upungufu wa rasilimali watu.
Aidha, alisema wamekwisha endesha mafunzo endelevu kwa wataalam hao ili waweze
kutoa huduma bora.
Alitaja huduma nyingine
wanayotoa ni ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda
kwa mtoto kwa kuhakikisha mama anazaa vizuri na mtoto anazaliwa salama bila ya
maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Taasisi
ya MDH imeanza kazi zake nchni Tanzania tangu mwaka 2000 kwa hisani ya full shangwe blog.