SPIKA WA BUNGE AWASILI CANADA MJINI QUEBEC
Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika uwanja wa ndege
mjini Quebec, Canada tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 127 wa chama cha
Mabunge Duniani (IPU) unaotarajia kufunguliwa rasmi kesho tarehe 21
Oktoba, 2012 na kumalizika 26 Oktoba . Makinda ameongoja ujumbe wa
wabunge wanne kutoka Tanzania, ambapo zaidi ya maspika wa nchi 150
duniani wakiongoza ujumbe wa wabunge kutoka Nchi zao watashiriki mkutano
huo.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiteta jambo kuhusu maandalizi ya awali
ya mkutano na afisa kutoka Bunge la Canada mara alipopokelewa baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege mjini Canada kuhudhuria mkutano wa 127
wa Chama cha Mabunge Duniani. Kulia ni Mhe. David Kafulila na Mhe. Hamad
Rashid waliongozana na Mhe. Spika katika Mkutano huo nchini Canada
Mhe.
Spika Anne makinda na ujumbe wake wakionyesha nyaraka muhimu za
kusafiria kwa ofisa wa uwanja wa ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege baada ya kuwasili mjini Quebec nchini Canada kuhudhuria Mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU)