YANGA, RUVU SHOOTING YAINGIZA TSH MIL 47/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga
na Ruvu Shooting lililochezwa jana (Oktoba 20 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa wenyeji Yanga kushinda mabao 3-2
limeingiza sh. 47,615,000.
Watazamaji 8,233 walikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000, na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
8,420,578.47 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
7,263,305.08.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 203,000,
waamuzi sh. 381,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, usafi na ulinzi wa
uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh.
2,000,000.
Umeme sh. 300,000, maandalizi ya
uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000
wakati tiketi ni sh. 2,959,100. Gharama za mchezo sh. 2,806,859.49,
uwanja sh. 2,806,859.49, Kamati ya Ligi sh. 2,806,859.49, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,684,115.69 na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,122,743.80.