MISS TABATA LEO
Shindano la kusaka Miss Tabata 2012 linafanyika leo (Ijumaa) katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu
wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa bendi za Mashauzi
Classic na Mashujaa zitawasindikiza warembo 19 watakaopanda jukwaani
kuwania taji hilo.
Mratibu
wa shindano hilo lililoandaliwa na Bob Entertainment na Keen
Arts alisema kuwa mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh 500,000/- na
king’amuzi ambayo imelipia miezi sita yenye thamani ya sh 800,000
iliyotolewa na Multichoice.
Mshindi wa pili atapata sh 500,000, mshindi wa tatu sh 350,000 wakati washindi wa nne na watano kila moja atapata sh 200,000.
Kapinga alisema warembo watano watawakilisha Tabata kwenye shindano la Miss Ilala.
Warembo wengine watakaoingia 10 bora kila moja atapata sh 100,000 wakati waliyosalia watapata Sh 50,000 kila moja.
Kapinga alisema shindano hilo pia litatumika kwa ajili ya kusherehekea miaka 10 tangu kuasisiwa kwa shindano la Miss Tabata.
“Shindano
la mwaka huu sio la kukosa kwani litakuwa ni la aina yake ukizingatia
kuwa litatumika kusherekea miaka 10 tangua kuanza kuandaa Miss Tabata,”
alisema Kapinga.
Alisema warembo waliyowahi kushinda mataji mbalimbali ya shindano hilo, pia wamealikwa kusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata.
Shindano
hili limedhaminiwa na Dodoma Wine, Redds, Integrated Communications,
Fredito Entertainment, Multichoice Tanzania, Screen Masters, Kitwe
General Traders, Step In Electronics, Brake Point, Atriums Hotel na Lady
Pepeta.
Mrembo anayeshikilia taji la Tabata kwa sasa ni Faiza Ally.
Warembo
wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania
ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya
kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds.