VIWANGO VYA SHULE VYA SHUSHWA
Ripoti ya kujitegemea ya
serikali ya Uingereza imebaini kwamba msaada wa Uingereza kwa nchi za
Afrika za Ethiopia, Rwanda na Tanzania umechangia kuporomoka kwa viwango
vya elimu katika shule za nchi hizo.
Uchunguzi umeonyesha kuwa watoto milioni hamsini
na mbili zaidi wanapata elimu kwa sababu ya msaada huo, huku walimu
wasio na sifa ya ualimu wakiajiriwa kukabiliana na ongezeko hilo la
wanafunzi.Hii ni kumaanisha kwamba kiwango cha elimu kwa ujumla katika mataifa hayo kimeshuka, huku watoto wengi wakimaliza elimu yao bila kujua kusoma wala kuandika na kuhesabu.
Malcolm Bruce ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya maendeleo ya kimataifa ya bunge la Uingereza na ameiambia BBC kwamba, ingawa imebainika kasoro hiyo, lakini ni muhimu msaada huo uendelee kutolewa kwa nchi hizo.