HASHEEM THABEET KUJENGA UWANJA WA KISASA WA MPIRA WA KIKAPU
Mkurugenzi
wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Lord Baden Powell, Kanali Idd
Kipingu akizungumza machache mbele ya wageni wake waliofika mapema leo
shuleni hapo kwa ajili ya kuangalia namna ya kujenga uwanja wa mchezo
wa mpira wa kikapu.
Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania, anayechezea timu ya Portland Trail Blazers ya Marekani kwenye Ligi ya NBA, Hasheem Thabeet akizungumza
jambo mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lord Baden Powell
Memorial High School,wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kiwanja cha mpira
wa kikapu shuleni hapo mapema leo Bagamoyo,nje kidogo ya jiji la
Dar,kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu
Tanzania, Phares Magesa.Hasheem Thabeet ameahidi kuwajengea uwanja wa mpira wa kikapu shuleni hapo.