AJARI
Gari la Fusso lililo sababisha Ajali hiyo
Namba za gari la Fusso
Toyota Rav 4 ikiwa imebamizwa vibaya na Fusso hilo
Gari la Rav 4 lilivyo haribika kwa nyuma
Namba za Gari la Rav 4
Fusso kwa nyuma
Fusso kwa Mbele
***********************************
Ajali Mbaya imetokea usiku huu iiyo husisha Gari la Fusso namba T 596 BUB pamoja na Rav 4 namba
T 675 ATK, Maeneo ya CCM Mkoani Mbeya.
Shahidi
aliye kuwepo eneo la tukio amedai ya kuwa Dereva wa Gari la mizigo
Fusso alikuwa mwendo kasi sana, na huku akijaribu kuyapita magari
mengine matano ambayo yalikuwa mbele yake. Wakati huo anaendelea
kuyapita magari hayo tayali dereva wa Rav 4 alikuwa amesha washa taa
kuonesha kuwa anaelekea kulia na ndipo Dereva wa fusso akaligonga Gari
la Rav 4 ambalo baada ya hapo liliseleleka kwa umbali wa Takribani mita
300 kutoka usawa wa sehemu ambapo liligongewa.
Hata hivyo dereva wa Fusso aliyesababisha Ajali hiyo amekimbia eneo hilo. Hakuna aliye umia wala kupata majeruhi.