MAXIMO KUJA JANGWANI?
Aliyewahi
kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Marcio Maximo,
anatarajia kutua nchini wiki ijayo kwa ajili ya kutua Klabu ya Yanga na
kuchukua mikoba ya Kocha anayemaliza muda wake katika Klabu ya Yanga ya
jijini Dar es Salaam imeelezwa.
Kocha
huyo anatarajia kuwasili nchini akiwa na Kocha msaidizi wa Viungo, huku
akiwa ameongozana na mkewe kutokana na kuwa nashughuli pevu ya
kukiandaa kikosi hicho cha Yanga kinachotarajia kushiriki michuano ya
Kombe la Kagame.
Aidha
imeelezwa kuwa mara tu baada ya kupokea maombi ya kukinoa kikosi hicho
Maximo hakuwa na pingamizi lolote bali alikubaliana na maombi hayo moja
kwa moja huku akitoa mapendekezo ya kuwasajili wachezaji awatakao kwa
ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Katika
mapendekezo hayo ya wachezaji aliowahitaji Maximo ni pamoja na Beki wa
Simba, ambaye hadi sasa bado anazua gumzo na mtafaruku mkubwa baina ya
Klabu hizo mbili za watani wa jadi Simba na Yanga, Kelvin Yondan, pamoja
na Kipa Ali Mustapha 'Bartez'.
Chanzo
cha habari hizi kutoka Klabu hiyo ya Jangwani kimetonya kuwa baadhi ya
wachezaji wengine waliokwishamwaga wino katika Klabu hiyo kwa ajili ya
msimu ujao ni pamoja na, Beki wa timu ya Kagera Sugar, David Luhende,
mchezaji anayecheza soka la kulipwa na timu ya DC Motema Pembe, Mussa
Hassan Mgosi, Owen Kasule, kutoka Klabu ya Hoang Anh Gia Lai, ya
Vientnam, Middie Kagere, kutoka timu ya Polisi Rwanda na mchezaji wa
Tanzania, anayecheza Soka la kulipwa nchini Canada, Nizar Khalfan,
pamoja na Said Bahanuzi na Juma Abdul kutoka timu ya Mtibwa Sugar.
Aidha
imeelezwa kuwa Kipa huyo anayehitajika na Kocha mpya Maximo, 'Bartez'
tayari amekwisha saini mktaba na Klabu hiyo, huku Kipa namba tatu wa
timu hiyo, Shaban Kado, akiachiwa kwa Mkopo kurejea katika kikosi cha
timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.