NGOWI KUONGOZA KAMATI YA KUONGOZA YA KUANDAA MKUTANO 30 WA SHIRIKISHO MWAKANI
Kushoto
ni Rais wa IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba
ya Uajemi Onesmo Ngowi akimkabidhi cheti cha kutukuka Rais wa Shirikisho
hilo duniani Daryl Peoples wa Marekani katika sherehe iliyofanyika
kwenye Hotel ya Hawaiian Hilton Village Resort, jijini Hawaii, nchini
Marekani.
Habari na picha zimetumwa toka katika jiji la Honolulu, Hawaii, Marekani
Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa na Chama cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA)
limeteua Rais wa Shirikisho hilo katika bara la Afrika, Mashariki ya
Kati na Ghuba ya Uajemi, Mtanzania
Onesmo Ngowi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kuandaa mkutano wa 30 wa
Shirikisho hilo mwakani. Mkutano wa 30 wa IBF/USBA unatarajia kufanyika
katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia tarehe 24 hadi 30 Juni
mwaka 2013.
Ngowi
alichaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho la IBF/USBA
uliomalizika Hilton Hawaiian Village Resort, jinini Honolulu, Hawaii,
Marekani tarehe 2 Juni. Uteuzi wa Ngowi unafuatia juhudi zake
alizozifanya kuendeleza shirikisho hilo katika bara la Afrika tangu
ateuliwe na Rais wa zamani wa IBF/USBA Robert Lee Sr. mwaka 1999 jijini
New Jersey, Marekani. Onesmo Ngowi anakuwa mtu wa kwanza kutoka katika
bara la Afrika kushika nyadhifa kubwa katika taasisi ya ngumi duniani na
hii inaisaidia sana Tanzania na bara zima la Afrika kijitangaza vyema
katika nyanja mbalimbali kama vile Utalii na bishara.
Katika Kamati hiyo ya maandalizi kuna wajumbe sita nao ni ; Louis Priluker wa Marekani, Roberto Rea wa Italia, Lahcen Oumghar wa Uholanzina Roberto Ramirez wa Mexico.
Kamati hiyo itafanya shughuli zake katika kipindi cha mwaka mmoja na
itakutana mara 4 kwa mwaka. Sekretarieti ya Kamati ya Ngowi itakuwa
katika jiji la New Jersey nchini Marekani kuliko na makao makuu ya
shirikisho hilo duniani.
Jiji
la Berlin linasifika kwa uzuri wanndari zake pamoja na kuwa jiji la
biashara la kimataifa katika bara la Ulaya. Mkutano huo ulianzimia
kufanya mkutano wa IBF kwaka 2014 katika bara la Asia na mwaka 2015 IBF
itafanya mkutano wake ktika bara la Afrika mahali ambapo patateuliwa.
Ngowi anawahimiza
Watanzania ambao wako katika uandaaji wa mikutano kuchangamkia nafasi
hii ambayo itawaleta watalii zaidi ya 1000 nchini toka nchi zaidi ya 200
duniani. Hii ni nafasi ya nadra sana katika biashara na watanzania ni
muhimu wakachangamka kama wenzao wengine katika nchi zinazokuwa wenyeji
wa mikutano kama hii.