MKAZI WA MBEYA KAMA ALIVYOKUTWA JANA
Muuza Miwa maarufu akiwa anakatiza West Street jijini Mbeya mapema leo
Muuza Miwa maarufu akiwa anapanga miwa yake leo
Miwa ikiwa tayali kwa ajili ya kufanyiwa mauzo leo
Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph mwaisango aliye vaa shati Jeupe akifanya mahojiano na Muuza miwa huyo
Muda mchache baada ya kufanya mazungumzo Wadau walianza nunua Miwa eneo hilo
Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango Kulia akiwa na muuza miwa Pamoja na mdau mwengine wakipata miwa kutoka kwa mdau
Baada ya Mazungumzo na Mbeya yetu mdau aliondoka zake
***********************
Mbeya
yetu leo katika Kodoa kodoa na Kamera yetu ilipaya bahati kuonana Live
na Bwana Mecky ambaye ni muuza Miwa maarufu jijini Mbeya. Ambapo alipo
hojiwa alisema "Kwa kweli miwa hii naifuata kule Usangu ambapo nanunulia
kwa bei ya kule kule, Lakini miwa hii pia huwa naisambaza hapa jijini
pamoja na vitongoji vyake". Aliongeza na kusema kuwa "Watu wengi
wanaidharau sana biashara hii ambayo inaniingizia kipato kikubwa"
Mwisho akamalizia kuwa "Nawashauri vijana wenzangu msilalamike kuwa
hakuna ajira wakati kazi zipo nyingi"
Baada ya hapo aliondoka zake