WANAWAKE KIJIJI CHA IFIGO MBEYA WADAI MAJI
WANAWAKE wa kijiji cha Ifiga kata ya Ijombe wilaya ya Mbeya mkoani
Mbeya wamedai kuwa tatizo la maji katika
kijiji hicho limeendelea kuwa sugu na kupelekea kutumia maji ya
kisima ambayo si safi na salama na kujikuta wakiendelea kukumbwa na
tatizo la ugonjwa wa kichocho .
Wakizungumza na timu ya wanahabari wanaharakati wa mtandao wa
jinsia Tanzania (TGNP) waliotembelea kijijini hapo leo wanawake hao
walisema kuwa kijiji hicho kutokana na
ukosefu wa huduma hiyo ya maji wamekuwa wakilazimika kuchota maji
katika kisima kimoja kilichoppo kijijini hapo ambacho maji yake si
lazima kwa afya za binadamu.
Alisema Sophia John
kuwa kisima hicho kimekuwa kikitumia na wakazi zaidi ya 2000
wa kijiji hicho na kuwa pamoja na kuwa maji hayo si salama baadhi ya
watu hasa watoto wamekuwa wakiyanywa pasipo kuchemcha hali
inayochangia kuongezeka kwa idadi ya
wagonjwa wa kichocho katika kijiji hicho.
John alisema kuwa mbali ya watoto wa kijiji hicho kukumbwa na
tatizo la ugonjwa wa kichocho kutokana na huduma hiyo ya maji
wanayoitumia kuwa si salama bado wamekuwa wakichangia mradi
wakiiomba serikali
kusaidia kutatua tatizo hilo bila mafanikio .
Kwani alisema wanananchi wa eneo hilo hasa wanawake na watoto
wamekuwa wakiathirika zaidi na tatizo la ukosefu wa maji kutokana na
kisima hicho kuwa mbali na makazi yao hivyo wakati mwingine kutumia
muda wa masaa manee hadi 6 kwenda kufuata huduma hiyo ya maji
Kisimani .
Alisema kuwa tatizo hilo limepelekea kasi ya wanawake kuzalisha
kupungua zaidi na kulazimika kuachiwa majukumu zaidi ya kulea familia
kwa kufanya kazi ya kusaka maji pamoja na shughuli nyingine za shamba
huku baadhi ya wanaume wao wakishinda katika vijiwe wakisubiri
kuhudumiwa na mwanamke.
Kwa upande wake Anna Mbalawala alisema kuwa tatizo hilo la maji
limeanza kujitokeza kati ya mwaka 2007 baada ya uongozi wa
Halmashauri ya mji wa Mbeya kuanza mchakato wa kuwa jiji na hivyo
kulazimika kuchukua mradi wa maji ambao ulichangiwa na wananchi wa
kijiji hicho pia kwa kuchimba mtaro wa maji kutoka kijijini hapo na
maji hayo kwenda kutumiwa na wakazi wa jiji la Mbeya.
“Hapa kijijini tulikuwa na maradi wa maji ambao tulikuiwa tukiutumia
kupitia shirika la DANIDA
ila toka mwaka 2007 mradi huo ulichukuliwa na jiji la Mbeya japo
sisi wakazi wa kijiji hiki ndio tupo jirani na chanzo cha maji na
tulishiriki kuchimba mtaro ….sasa hivi maji safi na salama tunapata
kwa wiki mara moja na siku nyingine zote tumekuwa tukitumia maji ya
kisima”
Frola Mlowezi (34) anadai kuwa kutokana na wananchi
wa kijiji hicho kutumia maji ya kisima ambayo si salama watoto wake
wawili wamekuwa wakitibiwa ugonjwa wa kichocho kutokana na kutumia
maji hayo ya kisima.
Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maji kijijini hapo Molis Selema alisema kuwa kabla ya mradi huo kuchukuliwa
na jiji mwaka 2007 kulikuwa na kamati ya watumiaji maji ambayo kwa sasa ilivunjwa baada ya jiji kuchukua maradi huo.
Alisema kuwa kabla ya mradi huo kuchukuliwa kata zinazozunguka mradi
huo zaidi ya tano zilipiga kura na kuonekana kata mbili za Idaba na
Ijombe kushindwa kutetea mradi huo hivyo kuchukuliwa na jiji na
wananchi wa kijiji cha Ifiga ambao ndio
walikuwa wakitegemea mradi huo kuendelea kukosa huduma hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Ifiga Raphael Syejele alithibitisha
kuwepo kwa tatizo hilo la maji kijijini hapo na kuwa ugonjwa huo wa
kichocho unachangiwa na huduma mbaya ya maji wanayotumia wananchi
wake .
Alisema kuwa kijiji hicho kina idadi ya watu 1175 wakiwemo watoto
748 na wazee 127 ambao pia apo hatarini kukumbwa na ugonjwa huo wa
kichocho kutokana na kunywa maji hayo.
Hata hivyo alisema kati ya wakazi wa kijiji hicho 636 ni wanawake
ambao ndio wamekuwa wakitegemewa zaidi katika familia kwa kutumia
kutafuta huduma hiyo ya maji.
Afisa
afya wa kito cha afya Ifiga hakuweza kupatikana ili kueleza ukubwa
wa tatizo hilo la ugonjwa
wa kichocho katika kijiji hicho,huku kwa upande wake mhadisi wa
maji wilaya ya Mbeya Bahati Haule alisema kuwa bado serikali
haina mpango wowote katika kijiji hicho kwa sasa katika kutatua kero
ya maji wakati baadhi ya vijiji kama Iwalanje mkakati wa kutatua
kero ya maji unafanyika.
Alisema kuwa hali ya upatikanaji wa maji safi kwa
sasa katika Halmashauri ya Mbeya ni chini ya aslimia 50 japo alisema
ipo mipango mbali mbali ya kutatua tatizo hilo baadhi ya maeneo huku
akidai kuwa mbali ya kijiji cha Ifiga kutumia maji ya kisima bado kijiji
cha Iwalanje pia wanatumia maji ya kisima.
Alisema tayari Halmashauri imepokea fedha kutoka benki ya Dunia kiasi
cha shilingi milioni 800 kwa ajili ya kutatua kero ya maji kijiji cha
Iwalanje huku akidai kwa Ifiga bado wanasubiri wahisani.