Warembo wanaotarajia kupanda jukwaani kuwania Taji la Miss Vyuo Vikuu 2012, siku ya Ijumaa wiki hii katika Ukumbi wa Maisha Club, wakipozi kwa picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge, wakati warembo hao walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge mjini Dodoma Leo, Julai 03, 2012
MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO
Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu. Wanawake wengi wanalalamika kuwa hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao . Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika, muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala. Wengi walioachana au kutalikiana nao walipitia njia hii pia. Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu. Njia za kukusaidia 1. ...