Airtel Rising Stars Tanzania yatoka sare na Burkina Fasso
Michuano ya Afrika Airtel Rising Stars Tanzania yatoka sare na Burkina Fasso
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Airtel Rising Stars kwa nchi
za Afrika, (leo hii) imetoka sare ya bao 1-1 na Burkina Fasso,katika
mchezo uliofanyika katika uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi.
Matokeo hayo yanaiweka Tanzania shakani kusonga mbele katika michuano
hiyo baada ya jana kuianza vibaya kwa kukubali kufungwa bao 1-0 na
Gabon katika mchezo wake wa kwanza. Kufuatia matokeo hayo Tanzania
inasubiri bahati tu ili kusonga mbele kwani sasa itabidi kushinda mchezo
wake wa mwisho utakaofanyika kesho 23/08/2012 dhidi ya Zambia na wakati
huo huo kuiombea Gabon iifungwe
na Zambia katika mchezo wao wa mwisho.
na Zambia katika mchezo wao wa mwisho.
Kila kundi itatoa timu moja kusonga mbele hatua ya robo fainali zinazotarajiwa kuanza kesho kutwa.
Katika mchezo wa jana, Burkina Fasso ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kushtukiza katika dakika ya kwanza ya kipindi cha pili na hivyo kuwafanya vijana hao wa Tanzania kutulia na kuanza kucheza pasi za
kuonana hali iliyozaa matunda dakika kumi baadaye.
Katika mchezo wa jana, Burkina Fasso ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kushtukiza katika dakika ya kwanza ya kipindi cha pili na hivyo kuwafanya vijana hao wa Tanzania kutulia na kuanza kucheza pasi za
kuonana hali iliyozaa matunda dakika kumi baadaye.
Goli la kusawazisha la Tanzania lilipachikwa kimiani na mshambuliaji
wake hatari Paulo Balama aliyepokea pasi akiwa kati ya uwanja na
kuchanja mbuga kuelekea langoni mwa wapinzani wao, ambapo kabla ya
kufunga aliwapunguza mabeki watatu na kisha kumlamba chenga kipa wa Burkina Fasso na kuachia kiki kali iliyokwenda moja kwa moja wavuni.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kocha na mkuu wa msafara wa timu ya Tanzania, Salum Madadi alisema vijana wake walicheza vizuri isipokuwa tatizo ni kutopata muda wa kutosha wa wachezaji wake kuzoeana hasa ikizingatiwa kuwa timu hiyo inaundwa na kombaini ya wachezaji kutoka mikoa sita tofauti.
"Kwa mfano mchezo wetu wa juzi dhidi ya Gabon vijana walicheza vizuri
sana pamoja na tatizo la kutozoeana hata hivyo waliweza kuwabana
wapinzani kwa muda mwingi na hata kufika langoni mwa wapinzani wetu kwa
kupiga mashuti kadhaa ila bahati haikua yetu tu," alisema Madadi.
Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa jana kwa wanaume ni Kenya kutoka sare ya 1-1 na Ghana, Malawi pia kutoka sare ya 1-1 na Madagascar, Nigeria kutoka sare ya 1-1 na Niger, Congo DRC kuichakaza Chad bao 5-0 na Zambia kuichapa Burkina Fasso 5-0. Kwa upande wa wanawake Congo DRC iliichakaza Burkina Fasso magoli 8-0, Ghana nayo ikaichapa Kenya bao 7-2, Chad ikaifunga Nigeria bao 1-0 na Uganda kuifunga Sierre Leone 3-0.
Michuano hiyo ya Airtel Rising Stars kwa ngazi ya Afrika iliyoanzishwa kwa lengo la kuibua vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, Inafikia kilele keshokutwa kwa bingwa kupatikana ambapo mshindi huyo atapata nafasi kwa wachezaji wa timu nzima kuhudhuria kliniki ya sokaya kimataifa itakayoendeshwa na jopo la makocha kutoka klabu ya Manchester United na Arsenal za Uingereza itakayofanyika kuanzia Agosti 26 hadi 30 mwaka huu jijini Nairobi