JESHI LA POLISI LATOA SIKU SABA KWA BAADHI YA ASKARI POLISI WANAODAIWA KUIBA MILIONI 150 ZILIZOPORWA
JESHI la Polisi limetoa siku saba kwa baadhi ya askari
kuzisalimisha fedha zipatazo sh milioni 150 wanazodaiwa kuiba, ambazo
zilizoporwa na majambazi Mtaa wa Mahiwa na Livingston jijini Dar es
Salaam juzi.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema
kutokana na tuhuma hizo jeshi hilo limeunda Jopo la wapelelezi ili
kujua ukweli wa madai hayo.
Alisema Jopo hilo litaundwa na
watu watano, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum, Ahmed
Msangi, atakayehakikisha kwamba muda mfupi inavyowezekana, ukweli
upatikane ili wananchi wajulishwe matokeo.