Serengeti Fiesta 2012 yaanza kwa kishindo mjini Moshi
Wasanii
machachari Bongo Move Wema Sepetu (kushoto) na Aunt Ezekiel wakicheza
muziki wa bongo Fleva uliokuwa ukishushwa na Msanii wa Bongofleva,Ferooz
katika uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Bhaaaaass! katika
Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi usiku huu. Tamasha hilo
limebamba ile mbaya.
Ferooz akiwa na mmoja wa mashabiki wake wakilishambulia jukwaa vilivyo.
Sehemu
ya wakazi wa mji wa Moshi wakiendelea kushuhudia makamuzi ya wasanii
mbalimbali wanaotumbuiza usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la
Serengeti Fiesta 2012.
Prezoo
akiwarusha mashabiki kibao (hawapo pichani) waliojitokeza jioni ya leo
kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Pichani
juu na chini ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya na mmoja wa shiriki wa
shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezoo akitumbuiza jukwaani usiku
huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja
wa chuo cha ushirika mjini Moshi.
Mmoja
wa wasanii wa hip hop Joh Makini akikamua vilivyo usiku huu mbele ya
umati mkubwa wa watu uliojitokeza kwenye uzinduzi wa tamasha la Fiesta.
Msanii mahiri wa bongofleva,Lina akiwa na densaz wake wakilishambulia jukwaa vilivyo.
Lina akiimba wimbo wake Yalaiti
Mkali mwingine wa hip hop Mwana FA akishusha mitindo huru.
Pichani
juu na chini Mwana FA akilishambulia jukwaa vilivyo kwa mitindo yake
huru iliyokuna vilivyo mashabiki wake,waliofika kwa wingi kwenye tamasha
la Serengeti Fiesta 2012.
Wasanii
wa nyota wa Filamu hapa nchini nao walijumuika kwa pamoja kwenye
uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,pichani jukwaani ni Wema
Sepetu,Jacob Steven a.k.a JB,pamoja na Aunt Ezekiel wakilisakata sebene.
Ray nae akilisakata sebene vilivyo.