Fernando Alonzo ashinda Langalanga Ulaya


Dereva wa magari ya Timu ya Ferrari Fernando Alonso amekua dereva wa kwanza kushinda mara mbili mwaka huu kwa ushindi wa kishindo kwenye mashindano ya Ulaya.
Fernando Alonso
Fernando Alonso
Yeye Alonzo alianza katika nafasi ya 11 kabla ya gari la usalama kuingilia mashindano kufuatia ajali lakini juhudi zake zilimuezesha kupambana hadi nafasi ya nne.
Aliweza kuongoza kufuatia mizengwe iliyotokea ndani ya kituo cha magari ya McLaren ambako wakati wa kubadili tairi na kuongezea mafuta Hamilton alipoteza zaidi ya sekundi 14 na kwa bahati nzuri dereva aliyekua akiongoza Sebastien Vettel akashindwa kumaliza mbio hizo.
ferrari
Ferrari la Alonso
Kimi Raikkonen alimaliza wa pili, il hali Hamilton akikwama ikisalia mizunguko miwili baada ya kukwaruzana na Pastor Maldonaldo wa timu ya magari ya Williams.
Hadi hapo Hamilton alikua akishikiliaa nafasi ya pili akijitahidi kumaliza katika nafasi hio licha ya tairi kuishilia kwa kasi na Maldonaldo alimuingilia na kulichana gari kiasi kwamba halingeweza kuendelea na mbio.
Ushindi wa Alonzo ni wa 29 ukimweka tangu aane kushiriki mbio za magari na unamuweka kileleni mwa Madereva bora akiwa na pointi 20, Mark Webber ni wa pili na Hamilton wa tatu, Vettel anashikilia nafasi ya nne akiwa nyuma ya Alonzo kwa tofauti ya pointi 26.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA