RAIS KIKWETE ATEMBELEA SHAMBA LA MFANO LA KIJIJI CHA KICHOPELO,BAHI,MKOANI DODOMA
Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete akikagua nyanya
na mazo mengine ya mboga pamoja na mizabibu katika shamba linalomilikiwa
na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade huko katika kijiji cha Chikopelo,wilaya
ya Bahi, Mkoani Dodoma leo asubuhi.Kushoto
ni mmoja wa wamiliki wa Shamba hilo Bwana Alon Hoven anayeshirikiana na Bwana
Dunstan Mrutu(hayupo pichani).shamba hilo linamwagiliwa kwa kutumia teknolojia ya matone(Drip irrigation system).
Mmoja wa Wamiliki wa Shamba la Mboga katika kijiji
cha Chikopelo Bwana Alon Hoven kimwonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baadhi
ya mazao yanayozalishwa kwa kutumia mbegu bora pamoja na teknolojia ya ya
umwagiliaji wa matone wakati Rais alipotembelea shamba hilo katika kijiji cha
Chikopelo, wilayani Bahi,mkoani Dodoma
leo asubuhi.Shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mia moja linamilikiwa na kampuni
ya kilimo ya Tendaji Trade chini ya Bwana Dunstan Mrutu na Alon Hoven raia wa
Israel.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Rais Kikwete alisifu
juhudi za wawekezaji hao kwa kutumia mbinu za kisasa za kilimo na kuwaasa
wanakijiji wa Chikopelo kujifunza mbinu bora za kilimo hicho cha mboga ili
waweze kupata ufanisi na kuboresha maisha yao. Rais Kikwete alitumia fursa hiyo
kuwaonya viongozi wa kijiji cha Chikopelo kutoendelea kuuza ardhi yote kwa
wawekezaji na badala yake kutunza na kuilinda kwaajili ya kizazi kijacho.
Awali katika salamu zao kwa Rais,Bwana Dunstan Mrutu na mmiliki mwenzake bwana Alon Hoven mbali na
kutoa ajira kwa wanakijiji hao waliahidi kushirikiana nao katika kujifunza
mbinu bora za kilimo na kuwawezesha kuzalisha mazao bora na mengi