WAREMBO MISS DAR INTERCOLLEGE WAFUNDWA
KAMATI ya Miss
TAnzania jana imetembelea kambi ya Miss Dar Intercollege iliyopo kwenye
hoteli ya The Grand Villa, Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kuwafunda.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika ijumaa ya kesho katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na chuo cha
Usmiamizi wa Fedha (IFM).
Akizungumza
na warembo hao, mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania Albert
Makoye aliwataka warembo hao kufuata miongozi na kanuni za shindano hilo
ikiwemo kuwa na nidhamu.
Alisema urembo si sura na umbo zuri bali unahusisha pia nidhamu katika jamii hivyo amewataka warembo hao kuzingatia hayo.
"Nafahamu
ninyi ni wasomi wazuri hivyo mmeyapokea vema mafunzo
tuliyowapa...hatutarajii kusikia mmoja wenu anachafua hali ya hewa
katika siku za usoni na mambo ya skendo skendo,"Alisema Makoye.
Dina alisema shindano hilo litapambwa na msanii wa uziki wa kizazi kipya nchini Nasib Addul ‘Diamond’ sambamba na bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema
katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo
watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE),
Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha
(IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya
kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga
fainali za Miss Tanzania.
Dina
aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose
Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema
Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha
Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano
hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen
Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada
Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za
Michuzi, dina ismail (zamani Mamapipiro), Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na
Fullshangwe.