MKUU WA WILAYA YA MERU ATOA WITO WA KUANZISHA KITUO CHA TELEVISHENI

MKUU wa wilaya ya Arumeru Bw Nyerembe Munasa ametoa changamoto kwa
halimashauri ya Meru na  manispaa  ya Arusha kuanzisha television
za halimashauri ambazo zitawawezesha kuandaa program ambazo
zitawaelekeza wananchi wao kutambua mambo muhimu yanayoendela
katika halimashauri zao pindi wawapo kwenye vikao

Bw. Nyerembe aliyasema hayo alipokuwa akiongea katika semina ya wadau
wa hlimashuri hizo ya  kuelimisha umma kuhusiana na mabadiliko ya
mfumo wa utangazaji kutoka analojia kwenda digital iliyofanyika mjini
hapa.
Bw. Nyerembe amesema kuwa  kutokana mabadiliko ya mafumo wa utangazaji
halimashauri zinapaswa kuhakikisha kuwa zinaanzisha television ambapo
kupitia mfumo huo zitawawezesha wananchi kuelewa mambo yanayoendelea
katika halimashauri zao pindi wawapo kwenye shughuli zao.

Aidha amewataka madiwani  wa halmashauri hizo kuhakkisha kuwa
wanasimamia kikamilifu miradi ya wananchi hao na kuhakikisha kuwa
wanawapa taarifa sahihi za mabadiliko ya mfumo wa utangazaji .

Mbali na hayo bw Nyerembe amewataka wananhabari kuanzisha vituo vya
utangazaji hasa kwa kipindi hiki cha mabadiliko ili waweze kujiajiri
wenyewe kwa kuwa waandishi  wao ndio mhimili wa nne wa dunia .

Pia ameeleza kuwa  waandishi wanapaswa kufanya utafiti kwa jamii juu
ya habari za kisayansi  na kuzitengenezea mkakati ya vipindi
vitakavyoleta mabadilikokwa jamii

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA