Jeshi la wanamaji la Italia limesema maharamia wamekwea na kuchukua udhibiti wa meli ya mafuta ya Italia katika bahari ya Hindi.
Meli ya Ujerumani ambayo pia imetekwa
Maharamia hao walifyatua risasi katika chombo kiitwacho Savina Caylyn, takriban kilomita 800 kutoka pwani ya Somalia.
Msemaji wa jeshi la wananamaji amesema hakuna aliyejeruhiwa miongoni mwa mabaharia 17 kutoka India na wataliano watano.
Maharama wamejipatia mamilioni ya dola
Msemaji wa jeshi la wanamaji la Umoja wa Ulaya
amesema shambulio la chombo hicho limefanyika katika eneo la mashariki
mwa kisiwa cha Yemen cha Socotra.
Meli hiyo imebeba shehena ya mafuta yaliyokuwa
yakipelekwa katika bandari ya Pasir Gudang nchini Malaysia, limeripoti
shirika la habari la Reuters.
Wanajeshi wa Marekani wakiwa na maharamia
Meli ya kivita ya Italia ilikuwa ikielekea
katika eneo la tukio, lakini iko umbali wa kilomita 600, na inatarajia
kuchukua siku kadhaa kuwasili, limeripoti shirika la habari la Italia.
Umoja wa Ulaya umesema meli hiyo imetekwa na mashua moja ikiwa na maharamia watano.
Maharamia wa Somalia
Msemaji wa jeshi la wanamaji wa Umoja wa Ulaya
amesema meli hiyo "ilikuwa ikielekea magharibi," upande wa pwani ya
Somalia, shirika la habari la AFP limekaririwa.
Maharamia wa Kisomali wametjipatia mamilioni ya
dola katika miaka ya hivi karibuni kwa kuteka meli za mizigo katika njia
inayotumiwa na meli katika pembe ya Afrika.