Posts

MDAU ARNOLD KAYANDA ANG'ARA

Image
Mdau Arnold Kayanda ameremeta na mke wake Aneth wakati wa sherehe yao. Arnold Kayanda akilishwa keki na wife wake. wazee wa kazi wakimeremeta. wanapendeza hawapendezi?. MC Kibonde akifanya vitu vyake.

MKE WA WAZIRI MKUU ATUNUKIWA SHAHADA NA MALECELA

Image
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, John Samwel Malecela akimtunuku Shahada ya Uongozi wa Biashara, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda katika Mahafali ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho Kibaha Oktoba 27, 2012.Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipokea zawadi ya ua kutoka wadogo zake Salma Rehani (kulia), Mkaroga Rehani (wapili kulia) na Mabe Rehani baada ya kutunukiwa Shahada ya Uongozi wa Biashara katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye vianja vya Chuo hicho, Kibaha Oktoba 27, 2012 ( Picha Ofisi ya Waziri Mkuu) Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa na baadhiimu wa mahafali hayo yaliyofanyika jana Kibaha mkoani Pwani Baadhi ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipowahutubia kwenye mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika Kibaha, Oktoba 27, 2012. (Picha na Of...

RAIS KIKWETE AANZA ZIARA YA MKOA WA KILIMANJARO HAPO JANA

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi mbalimbali na wananchi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro jana Oktoba 28, 2012 tayari kuanza ziara ya siku nne ya Mkoa wa Kilimanjaro akianzia Wilaya ya Same. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Agrey Marealemmoja wa viongozi wa chama cha mapinduzi CCM mkoani Kilimanjaro wakati alipolakiwa na viongozi mbalimbali na wananchi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro jana Oktoba 28, 2012 tayari kuanza ziara ya siku nne ya Mkoa wa Kilimanjaro akianzia Wilaya ya Same. Rais  Jakaya Kikwete akiangalia vikundi vya ngoma wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA jioni ya jana. Viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya Siasa wakimlaki Rais Jakaya Kikwete wakati alipowasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Rais jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi mbalimbali waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa kimat...

Rais Kikwete alishiriki Swala ya IDDI kijijini Msoga leo

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Iddi katika Masjid Rajab kijijini kwake Msoga-Chalinze leo Asubuhi. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa Iddi na baadhi ya waumini walishiriki swala ya Iddi katika Masjid Rajab Kijijini kwake Msoga, kata ya Chalinze,Wilayani Bagamoyo leo asubuh

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MSIKITI MPYA WA JIHAD WILAYA YA MWANGA-KILIMANJARO

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Jengo  la Msikiti mpya wa Jihad, baada ya kuzindua rasmi Msikiti huo uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa  Kilimanjaro, leo Oktoba 26, 2012 wakati wa Sikukuu ya Eid El Hajj, iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa  uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. Picha na  OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa Dini ya  Kiislam katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya  Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakat...

POLISI WAWATAJA WAUAJI WA KAMANDA BARO

Image
 Pichani kulia ni  Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumbaa akiyataja majina ya watuhumiwa hao wa mauaji ya Kamanda Barlo,na shoto ni IGP Said Mwema. JESHI la Polisi limewataja watuhumiwa 10, na bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine, ambao inadai walishiriki kumuua aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow. Kati ya watu hao watano wametiwa mbaroni Mwanza  na watu watano kutoka Dar es Salaam.  Leo (jana) mjini Mwanza, mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumba aliwataja watuhumiwa  hao ni Muganizi Michael Peter (36) mkazi wa Isamilo ambaye inadaiwa alikiri mwenyewe kumuua kamanda kwa risasi. Wengine ni Chacha Waitara Mwita (50), Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward Kusota na Bhoke Mara Mwita (42) ambao walikamatwa jijini Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego kwa msaada wa wananchi. Wanaoshikiliwa...

WARUDISHWA RUMANDE

Image
VIONGOZI WA UAMSHO WARUDISHWA TENA RUMANDE by John Bukuku on October 25, 2012 in JAMII with No comments Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Sheikh Farid Hadi Ahmed kushoto akiwa na wenzake sita walioletwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga wakiwa hawana ndevu na kufunguliwa mashtaka manne mapya mahakamani hapo yakiwemo kuharibu mali za watu zenye thamani ya Shl.Milioni 50 na kufanya vurugu za makusudi zakuhatarisha amani katika nchi…Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar Baadhi ya Askari wa kutuliza fujo wakiwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga kwa lengo la kutuliza amani Mahakamani hapo.. Picha na MakameMshenga-Maelezo Zanzibar Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO wakiwa wanatoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar Vuga baada ya kufunguliwa mashtaka manne mapya..Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Abdallah Juma kushoto na Salim Tawfik wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu kujitoa kwao sik...