Umoja blog ni blog ya kijamii,siasa,burudani na michezo
MDAU ARNOLD KAYANDA ANG'ARA
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Mdau Arnold Kayanda ameremeta na mke wake Aneth wakati wa sherehe yao. Arnold Kayanda akilishwa keki na wife wake.wazee wa kazi wakimeremeta.wanapendeza hawapendezi?.MC Kibonde akifanya vitu vyake.
Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu. Wanawake wengi wanalalamika kuwa hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao . Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika, muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala. Wengi walioachana au kutalikiana nao walipitia njia hii pia. Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu. Njia za kukusaidia 1. ...
Redds Miss Chang’ombe 2012, Catherine Masumbigana 21, (katikati) akipunga mkono mara baada ya kusimikwa rasmi kuwa mshindi wa taji hilo. Kulia ni mmshindi wa pili, Jesca Haule (18) na Mshindi wa tatu Zulfa Bundala. Masumbigana aliwashinda warembo wengine 13 katika shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Quality Center jijini Dar es Salaam Juni 10, 2012. Tano bora ya Miss Chang’ombe 2012 ambao wote wamepata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Temeke 2012 wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka Kushoto ni Zulfa Bundala (21), Jesca Haule (18), Catherine Masumbigana (21), Miriam Nkisigwa (20) na Flora Kazungu. Warembo wakicheza show maalum ya ufunguzi Vazi la ufukwenu, Kutoka kulia ni Restituta Faustiney, Wensley Mabula na Clara Diu. Warembo Flora Mayasa (kulia) Catherine Masumbigana (katikati) na Elizabeth Mushi wakiwinda point na vazi la ufukweni. Mkali wa Bongo Fleva Nassib Abdul 'Diamond' na vija...
Wachezaji, maafisa na mashabiki wamepata mapumziko mafupi katika fainali za ubingwa wa Ulaya,Jumatano ,(20.06.2012), lakini manung'uniko ya Ukraine ambayo ni mwenyeji mwenza wa mashindano haya yanaendelea. Ukraine wamejiunga na wenyeji wenza Poland kuwa ni pumba katika mashindano haya baada ya kushindwa kwa bao 1-0 dhidi ya Uingereza na gumzo lilituwama katika goli ambalo halikuwa, ambalo refa aliamua kuwa halikuvuka mstari lililofungwa na wenyeji hao dhidi ya Uingereza. Haki haikutendeka Hisia za kutotendewa haki nchini Ukraine hazikuweza kupozwa na Pierluigi Collina, mkuu wa waamuzi katika shirikisho la kandanda barani Ulaya Uefa, ...