Posts

AJALI YA TEGETA ILIVYOKUWA

Image
 Roli aina ya SICANIA lililokuwa limebeba mchanga likiwa limeacha njia na kuingia kwenye kwenye Bar ijulikanoyo kama Kmm maeneo ya Tegeta Kibaoni jijini Dar es salaam leo kwenye ajali hiyo mtu mmoja amefariki hapohapo na wengine wawili majeruhi. PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE Mabaki ya vifaa mbalimbali vilivyoharibiwa kwenye bar hiyo baada ya kutokea kwa ajali hiyo leo maeneo ya Tegeta. Jeshi la polisi likiimarisha ulinzi katika ajali hiyoiliyotokea leo maeneo ya Tegeta Kibaoni
Image
Deidre Lorenz na Rais wa IBF-USBA bala la Africa, Masharini ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi . Mcheza sinema toka Marekani Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amwasili leo na ndege ya Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zinazofanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka. Ujio wa Lorenz ambaye amecheza sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule, Perfect Strangers, The Big Fight umeleta msisimko mkubwa katika mji huu mkuu wa Kilimanjaro. Ujio wake umefuatia matayarisho ya muda mrefu ambayo yanaendana na hadhi yake. Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kumshuhudia mcheza sinema huyu, Lorenz alisema kuwa ameisikia kuwa mlima wa Kilimanjaro uko Kenya kwa kwa muda mrefu na ana furaha kubwa sana ya kufika ili kushughudia kuwa mlima huu maarufu duniani uko Tanzania. “Nimekuwa nautangaza sana ujio wangu kwenye blog na tovuti...

VIONGOZI WAPYA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

Image
Katibu Mkuu wa Ndani sport Club Jarahi Kilemile Akizungumza na wanamichezo na Watumishi Raia wa wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi baada ya kumchagua kuwa Katibu Mkuu wa Klabu hiyo.   Klabu ya Michezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Ndani Sports Club) imefanikiwa kupata Viongozi wake katika uchaguzi uliofanyika baada ya uongozi uliokuwepo kumaliza muda wake.   Viongozi waliochaguliwa ni Pamoja na Mwenyekiti Juma Katanga kutoka Idara ya wakimbizi, Katibu mkuu ni Jarahi Kilemile kutoka Idara ya Polisi na Mweka Hazina Daniel Njau kutoka idara ya Utawala ya mambo ya Ndani ya Nchi.   Uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na Uongozi wa TUGHE pia uliwachagua Viongozi watakao iwakilisha wizara kwenye SHIMIWI na Wajumbe wa Kamati Kuu ambapo idara zote zilishiriki.   Akiongea baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti Juma Katanga alisema atahakikisha anatumia Michezo kuitangaza wizara hiyo nakuhakikisha Timu za Wizara hiyo zinafanya vizuri...

Ureno nusu fainali Euro 2012

Image
Bao moja la Ronaldo limeiwezesha Ureno kuifunga Czech na kuingia nusu fainali Euro 2012 Mshambulizi Cristiano Ronaldo aliwaridhisha mashabiki wa Ureno kwa kucheza vizuri sana usiku wa Alhamisi, na juhudi zake kuiwezesha nchi yake kuishinda Jamhuri ya Czech bao 1-0 katika mechi ya mwanzo ya robo fainali ya Euro 2012, na kufanikiwa kuifikisha hadi nusu fainali. Ronaldo, ambaye alifunga magoli mawili wakati katika mechi ya awali ya mashindano hayo nchi yako ilipocheza na Uholanzi, aliweza kugonga mwamba katika nusu ya kwanza na ya pili katika mechi dhidi ya Jamhuri ya Czech. Hatimaye aliweza kuuelekeza mpira hadi wavuni kwa kichwa, huku zikiwa zimesalia dakika 12 kabla ya mechi kumalizika, na kipa Petr Cech akiweza kuufikia mpira, lakini hakuweza kuuzuia kutokana na nguvu nyingi zilizotumiwa na Ronaldo. Ilikuwa dhahiri kwamba wachezaj...

SIRI NZITO

Image
Sir Andy Chande akiwa na Rais Jakaya Kikwete. Andy Chande akiwa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa. ...Andy akiwa na Mzee Mwinyi. . ..Chande na Karume. ....Chande na Sumaye. Na Elvan Stambuli---Wa Gazeti la Uwazi. J AMII ya Siri (Secret Society), Freemason, imedaiwa kuwa na siri nzito na viongozi wakuu wa nchi yetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Madai hayo, yametokana na kile kinachoonekana kwamba Kiongozi Mkuu wa Freemason, Afrika Mashariki, Sir Andy Chande, amekuwa akijiweka karibu na viongozi wakuu wa nchi hii kila awamu, hivyo kuonesha kuwa kuna kitu anakitafuta. Kikubwa kinachodaiwa ni kuwa Chande anatumiwa na Freemason kuhakikisha kwamba kila kiongozi wa nchi hii anakuwa karibu na jamii hiyo ya siri. Inazidi kudaiwa kuwa Freemason inafanya njama za hali ya juu kujiweka karibu na Ikulu, ikiwa na mpango wao wa muda mrefu wa kusimika rais ambaye ni memba wa jamii hiyo katika awamu zinazokuja. Uchunguzi wa Uwazi umeones...

RAIS KIKWETE ATEMBELEA SHAMBA LA MFANO LA KIJIJI CHA KICHOPELO,BAHI,MKOANI DODOMA

Image
Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete akikagua   nyanya   na mazo mengine ya mboga pamoja na mizabibu katika shamba linalomilikiwa na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade huko katika kijiji cha Chikopelo,wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma   leo asubuhi.Kushoto ni mmoja wa wamiliki wa Shamba hilo Bwana Alon Hoven anayeshirikiana na Bwana Dunstan Mrutu(hayupo pichani).shamba hilo linamwagiliwa kwa kutumia teknolojia ya   matone(Drip irrigation system). Mmoja wa Wamiliki wa Shamba la Mboga katika kijiji cha Chikopelo Bwana Alon Hoven kimwonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baadhi ya mazao yanayozalishwa kwa kutumia mbegu bora pamoja na teknolojia ya ya umwagiliaji wa matone wakati Rais alipotembelea shamba hilo katika kijiji cha Chikopelo, wilayani Bahi,mkoani   Dodoma leo asubuhi.Shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mia moja linamilikiwa na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade chini ya Bwana Dunstan Mrutu na Alon Hoven raia wa Israel. Akizungumza wakati wa ziar...
Image
Mkutano Mkuu wa Dharura wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) utafanyika Juni 23 mwaka huu kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre, Dar es Salaam kuanzia saa 2.00 asubuhi.             Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa TWFA, Lina Kessy, ajenda kuu katika mkutano huo ni marekebisho ya Katiba ya chama hicho yanayotokana na maelekezo ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) juu ya marekebisho kwenye katiba za wanachama wake ambazo zina upungufu. Tayari mapendekezo ya marekebisho hayo kulingana na mwongozo wa TFF yalishapitiwa na Kamati ya Utendaji ya TWFA. Mbali ya Kamati ya Utendaji, wajumbe wengine wa mkutano huo ni Mwenyekiti, Katibu na mjumbe wa Mkutano Mkuu kutokana vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara. Wajumbe watafikia kwenye hosteli ya Msimbazi Centre ambapo wanatakiwa kuripoti siku moja kabla ya mkutano huo. Mgen...