VIONGOZI WAPYA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Katibu Mkuu wa Ndani sport Club Jarahi Kilemile Akizungumza na
wanamichezo na Watumishi Raia wa wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi baada
ya kumchagua kuwa Katibu Mkuu wa Klabu hiyo.
Klabu
ya Michezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Ndani Sports Club)
imefanikiwa kupata Viongozi wake katika uchaguzi uliofanyika baada ya
uongozi uliokuwepo kumaliza muda wake.
Viongozi waliochaguliwa ni Pamoja na Mwenyekiti Juma Katanga
kutoka Idara ya wakimbizi, Katibu mkuu ni Jarahi Kilemile kutoka Idara
ya Polisi na Mweka Hazina Daniel Njau kutoka idara ya Utawala ya mambo
ya Ndani ya Nchi.
Uchaguzi
huo ambao ulisimamiwa na Uongozi wa TUGHE pia uliwachagua Viongozi
watakao iwakilisha wizara kwenye SHIMIWI na Wajumbe wa Kamati Kuu ambapo
idara zote zilishiriki.
Akiongea baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti Juma Katanga
alisema atahakikisha anatumia Michezo kuitangaza wizara hiyo
nakuhakikisha Timu za Wizara hiyo zinafanya vizuri katika Michezo yote
watakayo shiriki.
Naye
Katibu Mkuu Jarahi Kilemile alisema Michezo katika wizara ya Mambo ya
Ndani ni muhimu na watumishi na wanamichezo wa wizara hiyo watarajie
uwakilishi mzuri na wenye kuleta mafanikio.
“Nitahakikisha
timu zetu zinafanya vizuri na kila mtumishi anayehitaji kushiriki
michezo anapata fursa hiyo kwakuwa michezo ni afya na lengo
nikuhakikisha tunakuwa na timu imara ambayo haisumbuliwi na wizara
nyingine yeyote”Alisema Kilemire.
Klabu hiyo inaundwa na watumishi raia na
wanamichezo kutoka Idara ya Polisi, Magereza,Uhamiaji,Wakimbizi, NIDA
pamoja idara ya Utawala ya wizara hiyo.