Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba kisiwani Zanzibar, Marehemu, Salim Hemed Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba Mbunge wa Chambani,Bwa.Salim Hemed Khamis,mara baada ya kuanguka ghafla hapo juzi jijini Dar akiwa katika vikao vya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya haraka. -- MAZISHI ya aliyekuwa Mbunge wa CUF, Jimbo la Chambani Pemba kisiwani Zanzibar, Marehemu, Salim Hemed Khamis,yanataraji kufanyika leo mchana mjini Pemba. Taarifa za awali kutoka Chama cha Wananchi CUF, zinasema kuwa Mwili wa Marehemu, Khamis utaagwa leo asubuhi kuanzia majira ya saa 2:30-4:00 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi mbalimbali wa kitaifa na Kimataifa pamoja na wananchi na Wanachama wa CUF watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu. Taarifa hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julis ...